Monday, January 5, 2015

RATIBA YA MZUNGUKO WA NNE WA KOMBE LA FA: UNITED, ARSENAL, CITY, CHELSEA WOTE WAPANGIWA VIBONDE.

RATIBA ya mzunguko wa nne wa michuano ya Kombe la FA imetolewa jana usiku, ambapo Manchester United wamepangwa kucheza ugenini dhidi ya timu ya daraja la pili ya Cambridge United. Mabingwa watetezi wa michuano hiyo Arsenal wao wamepangiwa kuifuata Brighton huku Chelsea nao wakipangiwa kucheza na mshindi kati ya Millwall au Bradford City. Mabingwa wa Ligi Kuu Manchester City wao watakuwa wenyeji wa Middlesbrough huku Aston Villa wakiikaribisha Bournemouth. Mechi nyingine ambayo itahusisha timu za Ligi Kuu ni Liverpool ambao wamepangiwa kucheza na Bolton Wanderers wakati mshindi kati ya Everton na West Ham United atasafiri kwenda kuchuana na mshindi kati ya Doncaster Rovers au Bristol City. Mechi hizi zinatarajiwa kuchezwa Januari 24 na 25 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment