KIUNGO wa klabu ya Cameroon, Stephane Mbia anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa siku 10 au 15 baada ya kupata majeruhi ya msuli. Mbia alipata majeraha hayo katika mchezo wa La Liga kati ya klabu yake ya Sevilla dhidi ya Celta Vigo Jumamosi iliyopita. Hata hivyo majeruhi hayo hayataweza kuzuia nafasi yake ya kuwemo katika kikosi cha timu ya taifa ya Cameroon kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika baadae mwezi huu. Mbia ana adhabu ya kufungiwa mechi moja na Shirikisho la Soka la Afrika-CAF, hivyo hatacheza mechi ya kwanza ya Afcon jambo ambalo litampa muda wa kutosha kupona. Nyota huyo ambaye ndiye nahodha wa kikosi hicho aliwaondoa hofu mashabiki wa Cameroon na kudai kuwa anaweza kuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa pili wa makundi ya michuano hiyo itakayofanyika huko Guinea ya Ikweta.

No comments:
Post a Comment