Monday, January 5, 2015

NEWCASTLE YASITISHA MKATABA WA BEN ARFA.

KLABU ya Newcastle United imesitisha mkataba wa kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Hatem Ben Arfa jana kufuiatia uhamisho wake kwenda klabu ya Nice. Klabu hiyo ilithibitisha leo kuwa tayari wameshafikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na kumtakia kila la heri popote atakapokwenda. Klabu ya Nice ilitangaza Jumamosi iliyopita kuwa Ben Arfa atafanyiwa vipimo vya afya leo. Ben Arfa alijiunga na Newcastle akitokea Olympique de Marseille mwaka 2010 lakini alishindwa kutamba baada ya meneja wa zamani Alan Pardew kuhoji kuhusu kiwango cha mchezaji huyo na moyo wake wa kujituma. Kiungo huyo alipelekwa kwa mkopo katika klabu ya Hull City mwanzoni mwa msimu lakini dili hilo lilitenguliwa mwezi uliopita kufuatia kushindwa kuelewana na meneja Steve Bruce.

No comments:

Post a Comment