MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2014 inayojulikana kama Ballon d’Or kwa mara ya pili mfululizo. Nahodha huyo Ureno amefanikiwa kushinda tuzo akiwazidi mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi na golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer. Kwa upande wa wanawake kiungo wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Wolfsburg ndiye aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwa wanawake huku kiungo wa kimataifa wa Colombia James Rodriquez akinyakuwa tuzo ya bao la mwaka. Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani aliyeiwezesha nchi hiyo kutwaa taji la Kombe la Dunia nchini Brazil mwaka jana Joachim Loew ndiye aliyeshinda tuzo ya kocha bora wa mwaka.
Mbali na tuzo pia kulikuwa na uteuzi wa kikosi bora cha mwaka ambapo wachezaji walioteuliwa ni pamoja na golikipa Neuer, mabeki ni Philipp Lahm, David Luiz, Thiago Silva na Sergio Ramos, viungo ni Andres Uniesta, Tony Kroos na Angel Di Maria huku washambuliaji wakiwa Arjen Robben pamoja na Messi na Ronaldo.


No comments:
Post a Comment