Saturday, January 10, 2015

SZCZESNY AMUANGUKIA WENGER KUFUATIA SOO LAKE LA KUVUTA SIGARA.

GOLIKIPA wa klabu ya Arsenal, Wojciech Szczesny amemuomba radhi bosi wake Arsenal Wenger kufuatia taarifa za nyota huyo wa kimataifa wa Poland kukutwa akivuta sigara bafuni baada ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton uliochezwa siku ya mwaka mpya. Wenger hakuthibitisha golikipa huyo kukutwa akivuta sigara lakini alidai kuwa amefanya makosa. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 65 amesema pamoja na kwamba amefanya makosa lakini wa kwanza kufanya hivyo na hatakuwa wa mwisho pia. Wenger amesema jambo la msingi ni mchezaji kutambua makosa yake na kujirekebisha kwani ndio sehemu ya ubinadamu.

No comments:

Post a Comment