Thursday, June 11, 2015

ADEBAYOR ADAI YUKO TAYARI KUITUMIKIA TOGO.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Togo, Emmanuel Adebayor amevunja ukimya na kudai kuwa anaweza kucheza mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika dhidi ya Liberia Jumapili hii. Nahodha huyo wa Togo pamoja na wenzake wawili walikataa kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo ambacho kiliitwa na kocha mpya Tom Saintfiet kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo bila kutoa taarifa yeyote. Adebayor ambaye alipewa likizo na klabu yake ya Tottenham Hotspurs kwenda kushughulikia matatizo yake ya kifamilia mwishoni mwa msimu, amedokeza kuwa amekuwa akifanya mazoezi binafsi baada ya kuitizama Togo akiwa jukwaani wakinyukwa bao 1-0 na Ghana katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jijini Accra. Akihojiwa kwanini hajajiunga na kikosi hicho, Adebayor amesema akifanya mazoezi binafsi kea ajili ya kujiweka fiti kwani alikuwa amekaa kipindi kirefu bila kucheza dakika tisini. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa kwasasa yuko fiti na yuko tayari kwa ajili ya mchezo Jumapili kama kocha atamuhitaji. Togo itakwaana na Liberia jijini Lome Jumapili mchana.

No comments:

Post a Comment