KLABU ya Barcelona wametawadhwa mabingwa wapya wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana baada ya kuibuka kidedea katika mchezo wa fainali dhidi ya mabinga wa Italia Juventus uliofanyika katika Uwanja wa Olimpiki jijini Berlin, Ujerumani.Mabao mahiri yaliyofungwa na Ivan Rakitic katika dakika ya nne, Luis Suarez dakika ya 68 na Neymar dakika ya tisini yalitosha kuihakikishia Barcelona taji lake la sita la michuano hiyo kwa kushinda mabao 3-1.
Akihojiwa mara baada ya mchezo huo meneja wa Barcelona Luis Enrique pamoja na kubainisha kuwa hajui mustakabali wake lakini amefurhishwa na mafanikio hayo ya muda mfupi aliyopata toka alipochukua kibarua hicho kutoka Gerardo Martino kiangazi mwaka jana.Naye meneja wa Juventus Massimiliano Allegri alikiri kuzidiwa maarifa na wapizania wao lakini amedai kuwa atajipanga vyema kuimarisha kikosi chake il msimu ujao waweze kutoa upinzani mkali zaidi.
No comments:
Post a Comment