Saturday, June 6, 2015

SERENA AENDELEA KUTAMBA TENISI WANAWAKE.

MWANADADA nyota wa tenisi wa Marekani Serena Williams ametawadhwa bingwa mpya wa michuano ya wazi ya Ufaransa baada ya kuibuka mshindi katka mchezo wa fainali dhidi ya Lucie Safarova.Williams mwenye umri wa miaka 33, alishinda taji hilo la tatu kwake kwa michuano hiyo kwa seti 2-1 zenye alama za 6-3 6-7 6-2.Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Williams alikiri kuwa michuano hiyo ilikuwa migumu kwake kwakuwa alicheza muda mwingi akiwa hayuko fiti kiafya asilimia mia moja.Kwa upande wa wanaume Novak Djokovic aliibuka kidedea na kutinga fainali ya michuano hiyo kwa kumchapa Andy Murray wa Uingereza katika mchezo ulioamuliwa kwa seti tano.Katika mchezo huo ulioanza Ijumaa na kukatishwa na hali mbaya ya hewa, Djokovic alishinda kwa alama 6-3 6-3 5-7 5-7 6-1, ambapo sasa atakwaana na Stan Wawrinka katika hatua ya fainali baadae.

No comments:

Post a Comment