Monday, June 8, 2015

LEBRON JAMES AIBEBA CAVALIERS KATIKA FAINALI YA PILI NBA.

MCHEZAJI nyota wa mpira wa kikapu wa Cleveland Cavaliers, LeBron James ameisaidia timu yake hiyo kuibuka na ushindi wa vikapu 95-93 dhidi ya Golden State Warriors na kufanya timu hizo kwenda sare ya kufungana mchezo mmoja mmoja katika fainali ya pili ya NBA. Katika mchezo huo James alifanikiwa kufunga vikapu 39, kudaka rebound 16 na kutoa pasi za mwisho 11. Akihojiwa James mwenye umri wa miaka 30, amesema alijitahidi kufanya kila analoweza kwa ajili ya timu na anashukuru kea ushirikiano aliopata kutoka kea wachezaji wenzake na kuepelekea kufanikisha ushindi huo muhimu. Katika fainali ya kwanza kati ya saba ambazo timu hizo zitacheza, Warriors walifanikiwa kuibuka na ushindi wa vikapu 108-100.

No comments:

Post a Comment