Monday, December 7, 2015

CARZOLA KUKAA NJE MIEZI MINNE.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa kiungo wake muhimu Santi Cazorla atafanyiwa upasuaji wa goti na anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitatu. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 30, aliumia mapema katika kipindi cha pili kwenye mchezo waliotoa sare dhidi ya Norwich City mwishoni mwa wiki iliyopita lakini aliendelea kubakia uwanjani mpaka mchezo ulipomalizika. Ilikuwa haiko wazi mara ya kwanza kama kiungo wa zamani wa Malaga angefanyiwa upasuaji au la, lakini baada ya mchezo wa juzi ambao Arsenal ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Sunderland, Wenger alithibitisha kuwa Cazorla atakaa nje mpaka Machi mwakani baada ya kufanyiwa upasuaji Ijumaa iliyopita. Akihojiwa Wenger amesema hivi sasa wanafahamu kuwa Cazorla hatakaa nje ya uwanja kwa msimu mzima kama ilivyodhaniwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment