Tuesday, December 8, 2015

CITY KUMKOSA KOMPANY.

NAHODHA wa Manchester City Vincent Kompany anatarajiwa kuukosa mchezo wa mwisho wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach kutokana na majeruhi ya kigimbi cha mguu. Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 amekuwa nje ya uwanjani kutokana na matatizo hayo toka mapema mwezi Novemba. Mshambuliaji Sergio Aguero, beki Martin Demichelis na kiungo Samir Nasri wote nao bado ni majeruhi. City tayari imejihakikishia nafasi ya kucheza hatua ya timu 16 bora lakini wanaweza kuwapita mabingw awa Italia Juventus na kuchukua uongozi wa kundi lao kama wakishinda huo.

No comments:

Post a Comment