Tuesday, December 8, 2015

SIERRA LEONE YARUHUSIWA TENA KUANDAA MECHI ZA KIMATAIFA BAADA YA EBOLA KUISHA.

SIERRA Leone sasa inaweza kuandaa michezo ya kimataifa kufuatia nchi hiyo kumaliza tatizo la maradhi ya Ebola. Shirikisho la Soka la Afrika-CAF liliifungia Sierra Leone kucheza mechi zake za kimataifa nyumbani kufuatia ushauri uliokuwa umetolewa na Shirika la Afya Duniani-WHO. Lakini umuzi huo uliokuwa umeanza kutumika Agosti mwaka jana, sasa umeondolewa kufuatia kumalizika kwa mlipuko wa maradhi ya Ebola kwa nchi za Magharibi mwa Afrika. CAF ililiarifu Shirikisho la Soka la nchi hiyo Desemba 6 kuhusu kupewa ruksa tena ya kuandaa mechi za kimataifa. Guinea na Liberia nazo pia zilisimamishwa kuandaa mechi za kimataifa kwasababu ya tishio la maradhi hayo katika nchi zao. Ebola nchini Sierra Leone imeua zaidi ya watu 4,000 kabla ya taifa hilo kutangaza kuutokomeza ugonjwa huo mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment