Sunday, December 13, 2015

MEZEMBE WATOLEWA ROBO FAINALI YA MICHUANO YA KLABU BINGWA YA DUNIA.

NDOTO za klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC kufika fainali nyingine ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia, zimezimwa kufuatia kutandikwa mabao 3-0 na Sanfrecce Hiroshima ya Japan katika mchezo wa robo fainali uliofanyika leo. Mabao ya Tsukasa Shiotani, Kazuhiko Chiba na Tkuma Asano yalitosha kuipa ushindi Hiroshima waliofuzu michuano hiyo kama wenyeji na kutiga hatua ya nusu fainali ambapo sasa watakwaana na mabingwa wa Afrika Kusini River Plate ya Argentina Jumatano ijayo. Mazembe mabingwa mara tano wa Afrika, waliweka historia mara ya mwisho kushiriki michuano hiyo miaka mitano iliyopita wakati walipoiondosha Internacional ya Brazil na kutinga fainali ambapo walifungwa na Inter Milan wakati huo ikinolewa na Rafa benitez. Katika mchezo huo Mazembe ambao waliwatumia wachezaji kutoka Ivory Coast, mali, Zambia, Tanzania, Ghana na mmoja kutoka DRC, walionyesha mchezo mzuri mwanzoni wakikosa nafasi kadhaa. Nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu aliyeingia kpindi cha pili walionyesha mchezo mzuri ingawa bahati haikuwa upande wao kwa kukosa nafasi kadhaa walizopata ambazo zingeipa timu yao ushindi.

No comments:

Post a Comment