Monday, December 14, 2015

MOURINHO AWAPIGIA DEBE MAKOCHA WAZAWA UINGEREZA.

MENEJA wa Chelsea, Jose Mourinho ameonya uwepo wa makocha wengi wa kigeni katika Ligi Kuu na kudai kuwaonea huruma makocha wazawa. Mourinho anainoa Chelsea kwa mara ya pili baada ya kuwafundisha mabingwa hao wa Uingereza kuanzia mwaka 2004 mpaka 2007 kabla ya kurejea tena mwaka 2013 na kuipa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita. Chelsea inakabiliwa na mchezo dhidi ya Leicester City baadae leo ambayo inanolewa na Claudio Ranieri raia wa Italia. Akihojiwa Mourinho amesema hivi sasa kuna makocha wengi wa kigeni katika Ligi Kuu kulinganisha na wakocha wazawa ambo ambalo anadhani linapaswa kutazamwa upya ili kutoa nafasi nyingi zaidi ya wazawa. Kwa sasa Ligi Kuu ina timu 20 na 12 kati ya hizo zinafundishwa na makocha wa kigeni huku nane zilizobaki zikifundishwa na makocha wazawa.

No comments:

Post a Comment