MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Neymar amekosa mazoezi ya timu yake leo wakati wakijiandaa na mchezo wao wa nusu fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia dhidi ya Guangzhou Evergrande. Mabingwa hao wa Ulaya na Hispania watakwaana na timu hiyo kutoka China mchezo ambao utafanyika jijini Yokohama, Japan Alhamisi hii. Neymar ambaye ni nahodha wa Brazil, anategemewa kuukosa mchezo huo kutokana na matatizo ya nyonga yanayomsumbua lakini anaweza kuwepo katika mchezo wa fainali Jumapili ijayo kama barcelona wakifuzu. Neymar ambaye yupo katika orodha ya majina matatu ya mwisho ya wachezaji watakaogombea tuzo ya Ballon d’Or mwakani, amefunga mabao 16 katika mechi 18 za mashindano yote alizocheza msimu huu.

No comments:
Post a Comment