Wednesday, December 9, 2015

WENGER AJIPA MATUMAINI YA KUFUZU CHAMPIONS LEAGUE.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amekubali kikosi chake kinapaswa kuvuka kikwazo kilichoko mbele yao baadae leo kama wanataka kufuzu hatua ya timu 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Arsenal wanatakiwa kuifunga Olympiakos kwa mabao 2-0 au kuwafunga mabao zaidi ya matatu ili waweze kusonga mbele. Lakini kazi haiwezi kuwa rahisi kwani Olympiakos kwasasa wako katika kiwango kizuri wakiwa hawajafungwa katika mechi zao zote za ligi walizocheza msimu huu huku wakiwa wameifunga Arsenal mabao 3-2 katika Uwanja wa Emirates Septemba mwaka huu. Akihojiwa Wenger amesema anafahamu ugumu waliokuwa nao mbele yao lakini ana uhakika wanaweza kuvuka kikwazo hicho na kusonga mbele.

No comments:

Post a Comment