Monday, January 18, 2016

NORWICH YAMNASA KLOSE.

KLABU ya Norwich City imefanikiwa kumsajili beki wa kimataifa wa Uswisi Timm Klose kutoka klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani kwa ada ambayo haikuwekwa wazi. Klose mwenye umri wa miaka 27 amejiunga na Norwich kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu akiwa amecheza mechi 39 za mashindano yote akiwa na klabu hiyo ya Bundesliga. Meneja wa Norwich, Alex Neil amesema Klose kama mchezaji amekuwa akitumia mbinu bora na pia ni mzuri wa mipira. Huo unakuwa usajili wan ne kufanywa na Norwich kipindi hiki cha Januari baada ya Matt Jarvis, Ivo Pinto na Ben Godfrey.

No comments:

Post a Comment