BEKI wa zamani wa kimataifa wa Serbia, Nemanja Vidic amesitishiwa mkataba wake katika klabu ya Inter Milan baada ya kushindwa kucheza mechi yeyote msimu huu. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Inter akiwa mchezaji huru akitokea Manchester United mwaka 2014 na kufanikiwa kucheza mechi 28 msimu uliopita. Vidic aliwashukuru viongozi, wachezaji na mashabiki wa Inter kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote na kuwatakia kila la kheri katika siku zijazo. Vidic amewahi kunyakuwa mataji matano ya Ligi Kuu na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka nane na nusu ambayo amekuwa Old Trafford.
No comments:
Post a Comment