Monday, January 18, 2016

SAKHO ANUSURIKA AJALINI.

MSHAMBULIAJI wa West Ham United, Diafra Sakho amesalimika katika ajali bila majeraha baada ya kugonga gari lake la kifahari la Lamborghini jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Senegal alithibitisha kupata ajali hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter akituma ujumbe wa kushukuru kwa kutodhurika kufuatia tukio hilo. Sakho tayari alikuwa na majeruhi ya msuli ambayo yamemuweka pembeni mwa kikosi cha West Ham toka Desemba mwaka jana ambayo alipata wakati wa mchezo dhidi ya West Bromwich Albion. Sakho ameifungia West Ham mabao matano pekee msimu huu.

No comments:

Post a Comment