Tuesday, March 1, 2016

BALE MBIONI KUREJEA KIKOSI CHA KWANZA.

WINGA wa Real Madrid, Gareth Bale amerejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanza baada ya kukaa nje toka Januari kutokana na majerhi ya msuli wa kigimbi. Mara ya mwisho nyota huyo wa kimataifa wa Wales kuitumikia Madrid ilikuwa katika ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Sporting Gijon lakini pamoja na kuanza mazoezi hayo na kikosi cha kwanza bado kuna wasiwasi kama atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho dhidi ya Levante. Bale mwenye umri wa miaka 26, alikuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha meneja aliyeondoka Rafa Benitez na kocha wa sasa Zinedine Zidane ameendelea kumtumia nyota huyo katika kikosi chake. Majeruhi ndio yamekuwa kikwazo kikubwa kwa Bale msimu huu, akiwa ameshakosa mechi 14 kutokana na matatizo ya msuli ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment