MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola amesema kipigo cha kushtusha cha mabao 2-1 walichopata kutoka kwa Mainz katika Uwanja wa Allianz Arena kunathibitisha kuwa Bundesliga sio ya kudharauliwa. Kipigo hicho cha Bayern kimeipa ahueni Borussia Dortmund ambao walishinda mchezo wao wa ugenini jana kwa mabao 2-0 dhidi ya Darmstadt na kupunguza pengo la alama baina yao kubakia tano. Timu hizo mbili zinatarajiwa kukwaana na Jumamosi hii ambapo Dortmund wanaweza kupunguza zaidi pengo la alama na Guardiola amesema historia haiku upande wao. Akihojiwa Guardiola amesema katika mchezo wa jana imeonekana wazi kuwa hakuna kitu rahisi na hakuna timu katika Bundesliga iliyowahi kushinda taji la Bundesliga mara nne mfululizo. Guardiola aliendelea kudai kuwa Dortmund ni timu tofauti kulinganisha na ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita hivyo wanapaswa kujipanga vyema kwa ajili ya mchezo wao ujao.
No comments:
Post a Comment