Thursday, March 3, 2016

ZIDANE ATAMBA BAADA YA KIKOSI CHAKE KUBEBWA NA WACHEZAJI WASIO NA MAJINA.

MENEJA wa Real Madrid, Zinedine Zidane amewapongeza wachezaji wake baada ya kutumia wale wasio na uzoefu katika kikosi chake kilichocheza ugenini na Levante jana. Madrid walifanikiwa kushinda mabao 3-1 ambayo yalifungwa na Cristiano Ronaldo kwa penati, bao la kujifunga la kipa wa Levante Diego Marino na Isco aliyefunga la tatu. Majeruhi na adhabu yalimlazimisha Zidane kufanya mabadiliko katika kikosi chake cha kwanza na kuwaingiza Lukas Vasquez, Casemiro na Borja Moyoral na ameonyesha kufurahishwa na jinsi walivyocheza kulinganisha na mchezo wao waliofungwa na mahasimu wao Atletico Madrid. Akihojiwa Zidane amesema wakati unapofanya mabadiliko mengi katika kikosi siku zote unategemea mambo kuwa magumu zaidi lakini hali ilikuwa tofauti jana kwani waliona mchezo mzuri.

No comments:

Post a Comment