MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amedai kuingiwa na hofu kutokana na matokeo ya kikosi chake katika usiku ambao timu zote tatu zinazofukuzia ubingwa wa Ligi Kuu zilifungwa. Arsenal walichapwa mabao 2-1 na Swansea na kuwaacha katika nafasi ya tatu wakiwa alama sita nyuma ya vinara Leicester City na Wenger amesema lazima wajitume ili waanze kupata matokeo chanya tena. Wenger aliendelea kudai kuwa kushuka kwa kiwango kwa timu yake kunachangiwa kiasi na hali ya kutojiamini waliyonayo wachezaji wake. Kwa upande wa Tottenham Hotspurs nao walishindwa kupata nafasi ya kwenda kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kukubali kipigo cha mabao 1-0 kutoka kwa West Ham United. Vinara Leicester ambao walipata sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Bromwich Albion juzi, waliendelea kupata bahati jana kufuatia Manchester City nao kutandikwa mabao 3-0 na Liverpool.
No comments:
Post a Comment