Tuesday, March 15, 2016

NUSU FAINALI FA: EVERTON WAWASUBIRI UNITED AU WEST HAM, PALACE WAO KUWAVAA WABABE WA ARSENAL.

KLABU ya Everton inatarajiwa kupambana na Manchester United au West Ham United katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA wakatio Crystal Palace wao wakichuana na wababe wa Arsenal, Watford. Mechi hizo za hatua zinatarajiwa kuchezwa katika Uwanja wa Wembley Aprili 23 na 24 na mwaka huu. United wanatarajiwa kusafiri kwenda Upton Park kwa ajili ya mchezo wa maruadiano war obo fainali dhidi ya West Ham baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo uliofanyika Old Trafford. Tarehe ya mchezo huo wa marudiano inatarajiwa kutangazwa baada ya mchezo wa mkondo wa pili wa michuano ya Europa League wa United dhidi ya Liverpool Alhamisi hii.

No comments:

Post a Comment