MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa watakosa huduma ya Petr Cech kwa zaidi ya wiki nne baada ya kipa huyo kupata majeruhi katika mchezo dhidi Swansea City juzi. Wenger anatarajia kuwakosa Cech na Laurent Koscielny katika mchezo dhidi ya mahasimu wao kutoka kaskazini mwa jijini London Tottenham Hotspurs kesho. Lakini sasa imebainika majeruhi ya kipa huyo wa zamani wa Chelsea yatamuweka nje kwa wiki tatu mpaka nne. Koscielny yeye anaendelea kuuguza majeruhi madogo aliyopata katika mchezo huo wa juzi na anategemewa kurejea Jumanne ijayo katika mchezo dhidi ya Hull City.
No comments:
Post a Comment