MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi uliopita wa Ligi Kuu huku meneja wa Leicester City Claudio Ranieri yeye akishinda tuzo ya kocha bora wa mwezi. Kane amefunga mabao matano mwezi uliopita, akifunga moja katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Arsenal na mengine mawili katika mchezo dhidi ya Aston Villa na Bournemouth. Mabao hayo aliyofunga nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza, yanamfanya kuongoza orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu akiwa na mabao 22, matatu zaidi ya Jamie Vardy. Kwa upande wa Ranieri yeye amepewa tuzo hiyo kutokana na kuisaidia Leicester kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama saba dhidi ya Spurs wanaoshika nafasi ya pili huku kukiwa kumebaki mechi sita.
No comments:
Post a Comment