MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Jamhuri ya Ireland na klabu ya Los Angeles Galaxy, Robbie Keane anatarajiwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti. Keane ambaye ndiye mfungaji bora wa kipindi chote wa Ireland akiwa amefunga mabao 67 katika mechi 143, alifanyiwa upasuaji huo jana. Nahodha huyo wa Galaxy anategemewa kukosa wiki mpaka sita baada ya upasuaji huo hivyo kumaanisha anaweza kuwa fiti kwa ajili ya michuano ya Euro 2016. Keane tayari ameshafunga mabao mawili katika Ligi Kuu ya Marekani-MLS msimu huu.
No comments:
Post a Comment