Friday, April 8, 2016

SUAREZ ASHUTUMIWA NA WAKALA WAKE WA ZAMANI.

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Luis Suarez ametuhumiwa kuwa na tatizo la kisaikologia na wakala wake wa zamani Daniel Fonseca ambaye amedai nyota huyo wa kimataifa wa Uruguay anamdai fedha zake. Suarez mwenye umri wa miaka 29, amesema katika mahojiano Jumanne iliyopita kuwa Fonseca anamdai asilimia 20 ya fedha ya ada ya uhamisho wakati alipotoka klabu ya Nacional kwenda Groningen mwaka 2006. Hata hivyo, Fonseca ambaye ni mchezaji wa zamani wa Uruguay amejibu madai ya Suarez na kumuona kama mtu mwoga kwa kudanganya. Fonseca aliendelea kudai kuwa Suarez ameonyesha kuwa na matatizo ya kisaikologia hivyo anahitaji kupatiwa huduma ya kitabibu.

No comments:

Post a Comment