Monday, August 1, 2016

MAHREZ AMCHANGANYA RANIERI.


MENEJA wa Leicester City Claudio Ranieri amekiri Riyad Mahrez anaweza kuwa amechanganywa na tetesi zinazomhusisha na yeye kwenda Arsenal kufuatia Arsene Wenger kudokeza kumuhitaji winga huyo. Taarifa zimekuwa zikizagaa kuwa Arsenal wanakaribia kukamilisha dili la kumsajili Mahrez mwenye umri wa miaka 25, lakini Ranieri amekanusha taarifa hizo akidai winga huyo wa kimataifa wa Algeria atabakia katika klabu hiyo. Hata hivyo, akihojiwa baada ya Leicester kuchapwa mabao 4-0 na Paris Saint-Germain katika mchezo wa kirafiki, Ranieri amesema anadhani mchezaji huyo amebadili mawazo. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Mahrez pengine atakuwa amechanganywa na tetesi zinazoendelea lakini angependa abaki.

No comments:

Post a Comment