Monday, August 1, 2016

MOYES ATAKA KUWACHUAKUA FELLAINI NA JANUZAJ.

MENEJA mpya wa Sunderland, David Moyes amethibitisha ni yake ya kutaka kuwasajili nyota wa Manchester United Marouane Felleini na Adnan Januzaj. Moyes, ambaye amechukua nafasi ya Sam Allardyce, ndio aliyemleta Fellaini nchini Uingereza wakati akiwa meneja wa Everton mwaka 2008 na baadae kumsajili wakati alipokwenda United mwaka 2013. Meneja huyo pia ndiye aliyempa nafasi Januzaj ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha United wakati akiinoa klabu hiyo na chipukizi huyo alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa kwanza ambao ulikuwa dhidi ya Sunderland Octoba mwaka 2013. Fellaini na Januzaj wanadaiwa kukosa nafasi chini ya meneja mpya Jose Mourinho na Moyes amethibitisha katika mkutano wake wa kwanza na wanahabari kuwa anataka kuwasajili wawili hao.

No comments:

Post a Comment