NAHODHA wa kimataifa wa Nigeria, Mikel John Obi amekanusha taarifa zilizozagaa kuwa anakaribia kuondoka Chelsea. Kiungo huyo amesema atabakia na kupigania nafasi yake na mkataba mpya katika klabu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge. Taarifa zilikuwa zimedai kuwa Mikel alikuwa akiwindwa na klabu kadhaa za China lakini mwenyewe amejitokea na kuweka wazi kuwa bado ataendelea kucheza soka Uingereza. Mikel amesema anataka kupigana ili kuisaidia timu yake kupata kila alama ili waweze kushinda mataji msimu ujao. Kwasasa Mikel yuko na kikosi cha Nigeria wakijiandaa kwa ajili ya michuano ya soka ya Olimpiki itakayofanyika huko nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment