KLABU ya Schalke imekubali kumsajili beki wa kulia wa Sevilla Coke kwa mkataba wa miaka mitatu. Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 ameichezea Sevilla kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kujiunga nao akitokea Rayo Vallecano mwaka 2011 na alifunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Liverpool katika fainali ya Europa League mei mwaka huu. Coke pia alikuwepo katika kikosi cha Sevilla kilichotwaa mataji ya Europa League kwa miaka miwili mfululizo akifunga katika bao kwa chamoto ya mikwaju ya penati katika fainali ya mwaka 2014 dhidi ya Benfica. Mkurugenzi wa michezo wa Schalke Christian Heidel alithibitisha taarifa kumnasa Coke na kudai kuwa atakuwa msaada mkubwa katika safu yao ya ulinzi msimu ujao.
No comments:
Post a Comment