RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani, Joao Havelange amefariki dunia jijini Rio de Janeiro akiwa na umri wa miaka 100. Havelange ndio rais wa kwanza asiyekuwa raia wa Ulaya kuliongoza shirikisho hilo kuanzia mwaka 1974 mpaka 1998, wakati nafasi yake ilipochukuliwa na Sepp Blatter nay eye kupewa urais wa heshima. Alijiuzulu nafasi hiyo ya urais wa heshima mwaka 2013 baada ya taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa kamati ya maadili ya FIFA Hans-Joachim Eckert kumtuhumu kupokea rushwa katika kipindi chake cha uongozi. Havelange aliwahi kushiriki michuano ya Olimpiki akiwa muogeleaji kutoka Brazil mwaka 1936 na alikuwa mmoja wa waogelaji katika timu ya polo huko Helsinki. Katika michuano ya Olimpiki iliyofanyika jijini Melbourne mwaka 1956, Havelange alikuwa kiongozi wa msafara wa Brazil kabla ya kujiunga na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC mwaka 1963. Havelange ndio mjumbe wa IOC aliyedumu kwa miaka mingi zaidi kabla ya kujizulu mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment