WAKALA wa kiungo wa Manchester City, Yaya Toure amesema mteja wake huyo amepanga kuendelea kubakia na kupigania nafasi yake katika kikosi cha timu hiyo pamoja na kuachwa katika mchezo wao wa kwanza wa msimu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ivory Coast ambaye alicheza chini meneja mpya Pep Guardiola wakati wakiwa Barcelona, aliondolewa katika kikosi kilichopata ushindi mwembamba wa bao 2-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu. Toure mwenye umri wa miaka 33 pia hatacheza katika mechi ya leo ya mtoano ya michuano ya Ligi Mabingwa Ulaya dhidi ya Steaua Bucharest ya Romania lakini wakala wake Dimitri Seluk amesema mteja amepania kubaki na kupigania nafasi yake. Akihojiwa Seluk amesema Guardiola ni kocha bora duniani na ana matumaini atampa Toure nafasi ya kuonyesha kuwa bado anaweza kuifanyia kitu City.
No comments:
Post a Comment