Tuesday, August 9, 2011

KWADWO ASAMOAH AACHWA KIKOSI CHA GHANA.


ACCRA,Ghana
KIUNGO Kwadwo Asamoah ameachwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kitakachocheza kesho.

Kwado ameondolewa kikosini kufuatia taarifa aliyoituma kutoka nchini Italia akiwa na klabu yake ya Udenise ambapo ameeleza kwamba amepatwa na maumivu wa kifundo cha mguu akiwa katika maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Hata hivyo wachezaji wengine walioitwa na kocha mkuu Goran Stevanovic kutoka nje ya bara la Afrika wameshawasili kambini na kesho wanatarajia kujumuyishwa kikosini.

Michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki kwa bara la Afrika itachezwa siku ya jumatano ambapo;

Senegal v Morocco, Dakar

Africa Kusini v Burkina Faso - Johannesburg

Gabon v Guinea - Paris

Equatorial Guinea v Guinea-Bissau - Lisbon

Zimbabwe v Zambia - Harare

Tunisia v Mali - Monastir

Ivory Coast v Israel - Geneva

Botswana v Kenya - Gaborone

Liberia v Angola - Monrovia

Malta v jamuhuri ya Afrika ya kati - Malta

The Gambia v DR Congo - Banjul

No comments:

Post a Comment