Tuesday, August 9, 2011

WENGER ANASA KINDA LA SOUTHAMPTON.


LONDON, England
WINGA kinda wa Southampton Alex Oxlade-Chamberlain amejiunga rasmi na Arsenal.

Kinda huyo wa England under 21, amejiunga na washika bunduki wa London kwa ada ya uhamisho £12million baada ya kufaulu vipimo vya afya.

Oxlade-Chamberlain, 17, ameishaichezea Southampton mechi 36 na akifunga magoli 10.

Chamberlain ambaye pia alikuwa akitakiwa na Manchester United na Liverpool anakuwa mchezaji wa 3 kusajiliwa na Arsenal baada ya kuwasili kwa Gervinho na Carl Jenkins

No comments:

Post a Comment