BALE HATARINI KUFUNGIWA.
 |
Gareth Bale. |
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amesema kuwa mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspurs Gareth Bale anaweza kukabiliwa na vikwazo kwa kuichezea klabu yake wakati wa mashindano ya Olimpiki ikiwa chama cha FA kitawasilisha malalamiko yake kuwa mchezaji huyo ameweza kuichezea klabu yake na kukataa kuichezea Timu ya Uingereza-GB. Bale alijiondoa kutoka timu ya GB inayojumuisha wachezaji kutoka kote Uingereza, Wales na Scotland kwa kudai majeruhi lakini mchezaji huyo alifunga bao la Spurs katika mchezo uliomalizika kwa sare ya 1-1 dhidi ya LA Galaxy katika ziara ya klabu hiyo nchini Marekani. FA na Kamati ya Olimpiki hazijatoa tamko lolote kuhusu kujitokeza kwa mchezaji huyo lakini Blatter anasema ikiwa chama hicho kitawasilisha malalamiko yao FIFA basi mchezaji huyo atawekewa vikwazo wakati wa olimpiki. Hata hivyo klabu ya Spurs inaweza kujitetea kwa kusema kua mchezaji huyo Bale alipata nafuu katika siku chache zilizopita, na hivyo kutetea uwamuzi wa mchezaji huyo kujiondoa kwenye kikosi cha GB.
No comments:
Post a Comment