Thursday, July 26, 2012

WAANDAAJI OLIMPIKI WAOMBA RADHI.

Luninga ya uwanjani ikionyesha picha ya mchezaji wa Korea Kaskazini huku pembeni kukiwa na bendera ya Korea Kusini.
WAANDAAJI wa michuano ya Olimpiki wameomba radhi kwa timu ya soka ya taifa ya wanawake ya Korea Kaskazini baada ya majina ya wachezaji wa timu hiyo kuonekana katika luninga ya uwanjani huku pembeni kukiwa na bendera ya Korea Kusini. Mara baada ya tukio hilo wachezaji wa nchi walitoka nje ya uwanja na kusababisha mchezo huo kuchelewa kwa muda wa saa moja kabla ya kuingia tena uwanjani na kuendelea na mchezo huo baada ya bendera yao kuwekwa. Katika mchezo huo ambao walikuwa kiacheza na Colombia, Korea Kaskani iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo huo wa kwanza kwenye michuano hiyo ambayo inatarajiwa kufunguliwa ramsi kesho. Kocha wa timu hiyo Gun Sin Ui ameonyesha kukerwa na kitendo hicho ambapo ameweka wazi kulipeleka suala hilo kwa waandaaji wa mchezo huo na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA. Katika michezo mingine ya wanawake iliyochezwa jana, Brazil ilifanikiwa kuifunga Cameroon kwa mabao 5-0, Sweden ikaifunga Afrika Kusini mabao 4-1, Japan ikashinda mabao 2-1 dhidi ya Canada, Marekani ikaifunga Ufaransa mabao 4-2 huku wenyeji wa michuano hiyo kombaini ya Uingereza ikiifunga New Zealand bao 1-0.

No comments:

Post a Comment