Tuesday, September 11, 2012

DROGBA ATUNUKIWA TUZO UFARANSA.


NAHODHA wa timu ya taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba ametajwa kama mshindi wa tuzo mchezaji mwenye kipaji kwa mwaka huu inayotolewa na luninga ya Canal Plus ya nchini Ufaransa. Tuzo hiyo ambayo hutunikiwa wachezaji kutoka Afrika ambao wametoa mchango mkubwa katika msimu kwenye moja ya ligi tano za juu barani Ulaya. Kamati inayoandaa tuzo hizo imemteua mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea kutokana na mchango wake alioonyesha katika timu yake hiyo msimu uliopita na kuiwezesha kunyakuwa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya. Drogba alikuwa akichuana na mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal Papiss Demba Cisse ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita.

No comments:

Post a Comment