MCHEZA tenisi nyota kutoka Uingereza, Andy Murray amefanikiwa kukata kiu ya miaka 76 na muingereza wa kwanza kutwaa taji la Grand Slam baada ya kumfunga Novak Djokovic katika michuano ya wazi ya Marekani au US Open. Murray ambaye ana umri wa miaka 25, alifanikiwa kutwaa taji hilo ambalo mara ya mwisho Fred Perry alitwaa mwaka 1936, kwa kumfunga Djokovic kwa 7-6 7-5 2-6 3-6 6-2 akitumia muda wa saa nne na dakika 54 mchezo ambao ulifanyika katika Uwanja wa Arthur Ashe jijini New York. Mbali na taji hilo Murray pia aliingia katika fainali ya michuano ya Wimbledon na kushinda medali ya dhahabu katika michuano ya olimpiki iliyofanyika jijini London katika kipindi hiki cha kiangazi. Pamoja na mafanikio mengine aliyopata, ushindi wa michuano hiyo utakuwa ni kama changamoto kwa wachezaji wa mchezo huo nchini Uingereza bada ya kusubiria taji la Grand Slam kwa kipindi kirefu.

No comments:
Post a Comment