Saturday, September 8, 2012
NEYMAR AWASHANGAA MASHABIKI WA BRAZIL KUWAZOMEA.
MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Brazil, Neymar amewaponda mashabiki wa soka nchini humo baada ya timu yake kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Afrika Kusini jana. Nyota wa klabu ya Zenit St Petersburg, Hulk ambaye alifunga bao pekee la mchezo huo naye pia aliwashambulia mashabiki kushindwa kuishangilia timu yao hivyo kupunguza uwezo wao wa kujituma kwenye mchezo huo. Akihojiwa Neymar amesema kuwa anajua kuwa kikosi chao hakikuonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo lakini walifanikiwa kuibuka na ushindi, hivyo kusononeshwa na kitendo cha mashabiki kuwazomea katika mchezo huo. Neymar ameendelea kusema kuwa hana maana ya kuwaambi mashabiki wamshangilie lakini aliwaomba waishangilie timu yao ya taifa. Brazil inakabiliwa na mchezo mwingine wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya China Jumanne Septemba 11 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment