Monday, March 18, 2013
FA KUKUMBUKA TUKIO LA MUAMBA KWA KUONGEZA VIFAA VYA UOKOAJI.
CHAMA cha Soka nchini Uingereza-FA kinatarajia kutangaza kuongeza vifaa vya uokoaji zaidi ya 900 kwa ajili ya vilabu vya wanaume na wanawake nchini humo wakati wa mchezo wa Kombe la FA ikiwa ni kumbukumbu ya mwaka mmoja toka Fabrice Muamba alipozimia uwanjani. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo, mpango huo unatarajiwa kutoa maelfu ya vifaa hivyo kwa kuwapa wachezaji, maofisa na mashabiki uwezo wa kuvitumia na maelezo stahiki kwa ajili ya kuokoa maisha. FA kwa kushirikiana na Mfuko wa Moyo nchini humo-BHT wametoa kiasi cha paundi 400,000 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa hivyo huku paundi 400,000 zikiwa zimetolewa na vilabu. Tahadhari hiyo ya kujaribu kupambana na matatizo ya kusimama moyo ghafla imewekwa wakati Muamba alipoanguka ghfla na kuzimia wakati timu yake ya Bolton Wanderers ilipokuwa ikicheza na Tottenham Hotspurs katika mchezo wa Kombe la FA katika Uwanja wa White Hart Lane Machi 17 mwaka jana. Muamba ambaye baadaye alipona kabisa baada ya moyo wake kusimama kwa dakika 78, ameshastaafu kucheza soka kwa ushauri wa madaktari kwani hata kupona kwake imekuwa kama bahati kwasababu kati ya watu 10 wanaopata tatizo kama lake ni mmoja tu anayeweza kupona.
No comments:
Post a Comment