Monday, March 18, 2013
MCMANAMAN HATARINI KUFUNGIWA MECHI TATU.
MCHEZAJI wa Wigan Athletic Callum McManaman anatarajiwa kufungiwa mechi zipatazo tatu kutokana na faulo yake mbaya aliyomchezea beki wa Newcastle United Massadio Haidara katika mchezo wa Ligi Kuu uliokutanisha timu hizo jana. Chama cha Soka nchini Uingereza kinajipanga kumchukulia hatua mchezaji huyo baada ya mwamuzi wa mchezo huo Mark Halsey kushindwa kumwadhibu kwa kutoliona tukio hilo. Haidara mwenye umri wa miaka 20 ambaye alijiunga na klabu hiyo akitokea Nancy kwa mkataba wa miaka mitano kuanzia Januari mwaka huu aliumia goti lake kutokana na dhoruba aliyopewa na MacManaman. Mara baada ya faulo hiyo ya McManaman mchezo ulisimamishwa kwa muda wa dakika tano wakati Haidara akipatiwa matibabu uwanjani kabla ya kubebwa na kutolewa nje akiwa katika machela.
No comments:
Post a Comment