Sunday, March 17, 2013

FLAMENGO YAMTIMUA KOCHA WAKE.

KLABU maarufu na yenye mashabiki wengi zaidi nchini Brazil ya Flamengo imemtimua kocha wake Dorival Junior baada ya kugoma kupunguziwa mshahara wake. Katika taarifa iliyotumwa katika mtandao wa klabu hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya mazungumzo yaliyochukua miezi miwili yenye nia ya kuufanyia marekebisho mkataba wa kocha huyo aliosaini mwaka jana kushindwa. Junior mwenye umri wa miaka 50 ambaye amefundisha vilabu mbalimbali nchini humo ameinoa Flamengo kwa kipindi cha miezi tisa. Mwaka uliopita Flamengo ilishindwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wake kwa muda stahiki na uongozi mpya ambao umeingia madarakani Januari mwaka huu chini rais Eduardo Bandeira de Mello una nia ya kupunguza gharama katika uendeshaji wa klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment