Sunday, March 17, 2013
BADO NIPO NIPO - HEYNCKES.
MENEJA wa klabu ya Bayern Munich, Jupp Heynckes amedokeza kuwa anaweza asistaafu mwishoni mwa msimu huu pamoja na ujio wa kocha mpya Pep Guardiola katika klabu hiyo. Kumekuwa na tetesi kuwa kocha huyo mwenye umri wa miaka 68 anawezakuachana na mambo ya soka mwishoni mwa msimu lakini mwenyewe alizipuuza tetesi hizo kwa kudai kuwa bado ana muda mwingi wa kuendelea kufundisha. Kocha huyo amesema umri bado unamruhusu kuendelea kufundisha akitolea mfano viongozi wenye umri mkubwa zaidi yake ambao wamekuwa madarakani kama Chancellor wa zamani wa Ujerumani Konrad Adenauer ambaye alichukua madaraka akiwa na umri wa miaka 71 na sasa Papa mpya ambaye ana umri wa miaka 76. Kauli ya kocha huyo imekuja wakati akihojiwa baada ya mchezo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani maarufu kama Bundesliga dhidi ya Bayer Leverkusen uliochezwa katika Uwanja wa BayArena. Mchezo ambao Bayern iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kuendelea kujikita kilelei mwa msimamo wa ligi hiyo.
No comments:
Post a Comment