Sunday, March 17, 2013

SAMATTA AIBEBA TP MAZEMBE UGENINI.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta jana ameisaidia timu yake ya TP Mazembe ya jamhuri ya Kidemokasia ya Congo kwa kuifungia bao la ushindi katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya timu 32 bora dhidi ya Mochudi Centre Chiefs ya Botswana. Katika mchezo huo timu hizo mpaka kipindi cha mapumziko timu hizo zilishindwa kutambiana kwa kutofungana lakini Mazembe walitakiwa watoke kifua mbele baada ya beki wake Jean Kasusula kukosa mkwaju wa penati katika dakika ya 10 ya mchezo huo. Kipindi cha pili Mazembe walibadilika na kuonyesha kutafuta bao la ugenini na juhudi zao zilizaa matunda baada ya Samatta kufunga bao hilo zikiwa zimebaki dakika 10 kabla ya mpira kumalizika hivyo kuihakikishia ushindi timu hiyo. Mchezo wa marudiano baina ya timu hizo unatarajiwa kufanyika jijini Lubumbashi mapema mwezi April mwaka huu. Katika michezo mingine ya michuano hiyo iliyochezwa jana Tusker ya Kenya ililala kwa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly ya Misri, Zanaco fc ya Zambia ilishindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment