MCHEZAJI tenisi nyota Rafael Nadal wa Hispania amefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya wazi ya BNP Paribas baada ya kumfunga Tomas Berdych wa Jamhuri ya Czech katika hatua ya nusu fainali. Nadal ambaye amekaa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi saba alionyesha kuumudu vyema mchezo huo uliofanyika huko Indian Wells, California kwa kufanikiwa kumfunga Berdych kwa 6-4 7-5. Nyota huyo ambaye alimtoa hasimu wake wa siku nyingi Roger Federer wa Switzerland katika hatua ya robo fainali alionekana kurejea katika kiwango chake cha zamani baada ya kukaa nje kwa muda mrefu. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Nadal amesema wakati unapokuwa nje kwa kipindi kirefu huwa inakuwa ngumu kurejea katika kiwango chako cha kawaida lakini kama unashinda mara kwa mara kama anavyofanya inasaidia kuongeza kujiamini na kucheza kama alivyozoea zamani. Nadal sasa atachuana na Juan Martin del Porto wa Argentina katika hatua ya fainali baada ya muargetina huyo kumng’oa Novak Djokovic kwa 4-6 6-4 6-4 na kutinga hatua hiyo.
No comments:
Post a Comment