Thursday, April 4, 2013
ARMSTRONG KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUOGELEA.
MWENDESHA baiskeli kutoka Marekani, Lance Armstrong amepanga kurejea katika ulingo wa michezo akiwa kama muogeleaji. Armstrong mwenye umri wa miaka 41 ambaye alikumbwa na kashfa ya kutumia dawa za kuongeza nguvu na kunyang’anywa mataji yake yote saba ya mbio za baiskeli za Tour de France, alijiandikisha kushiriki mashindano ya kuogelea yatakayofanyika jijini Texas mwishoni mwa wiki hii. Wakala wa kupambana na dawa za kuongeza nguvu nchini Marekani-Usada, ambao mbali na kumvua mataji yake lakini pia walimfungia maisha kushiriki michuano yoyote ya baiskeli. Januari mwaka huu Armstrong alikiri kutumia dawa za kuongeza nguvu katika mataji yake yote saba ya Tour de France aliyonyakuwa katika kipindi cha mwaka 1999 mpaka 2005 katika mahojiano ya luninga na mtangazaji maarufu Oprah Winfrey.
No comments:
Post a Comment