VYOMBO vya habari nchini Cameroon vimeripoti kuwa polisi katika Uwanja wa Ndege wa Douala wamezuia pasi ya kusafiria ya rais wa Shirikisho la Soka nchini humo Iya Mohammed ambaye alikuwa akisafiri kuelekea nchini Ufaransa. Mohammed ambaye pia ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya umma ya katani-Sodecoton ameema likuwa akitaka kusafiri kuelekea jijini Paris, Ufaransa kwa ajili ya mkutano na alikuwa amekamilisha taratibu zote za safari wakati polisi wawili walipotokea na kudai wametumwa kumzuia asisafiri kwenda na kunyang’anya pasi yake. Amesema hakuna sababu yoyote aliyopewa kuhusiana na tukio hilo kwake zaidi ya kuchukua pasi yake na kuondoka nayo. Baraza la udhibiti wa bajeti na fedha, ambalo lilisimamia Sodecoton lilitoa taarifa Machi 29 mwaka huu wakimtuhumu Mohammed kwa matumizi mabaya ya ofisi ambayo yalipelekea kampuni hiyo kupata hasara ya dola milioni 18.
No comments:
Post a Comment