Saturday, May 4, 2013
BARCELONA ILIFANYA MAKOSA KUMUAJIRI VILANOVA.
RAIS wa zamani wa klabu ya Barcelona, Joan Laporta anaamini kuwa klabu hiyo ilifanya uamuzi usiokuwa sahihi kumteua Tito Vilanova kama kocha mkuu mwanzoni mwa msimu wa 2012-2013. Vilanova mwenye umri wa miaka 44 alitajwa kuchukua nafasi ya Pep Guardiola na kupewa mkataba wa mwaka mmoja lakini Laporta anafikiri Vilanova hakuwa tayari kwa nafasi hiyo kwa kipindi kile. Laporta amesema walimteua Vilanova kwasababu walikuwa wanaogopa kuwa nani ataweza kuchukua nafasi ya Guardiola lakini ilikuwa mapema sana kufanya uamuzi huo. Laporta aliendelea kusema kuwa Barcelona walipaswa kutafuta mbadala wa kocha mwingine wakati Vilanova alipokuwa ameondoka kwa matibabu ya kansa nchini Marekani ingawa alikiri ungekuwa uamuzi mgumu kufanya hivyo ila kulikuwa hakuna jinsi.
No comments:
Post a Comment